Salam msomaji

Ni siku nyingi sana zimepita tangu nilipoandikia blog hii. Mizunguko ya kimaisha ya hapa na pale ilinifanya kuwa kimya sana. Nimekuja kuwatakia heri ya mwisho wa mwezi wa septemba na kuwatakia Baraka nyingi kwa mwezi oktoba. Oktoba ni mwezi muhimu sana kwa nchi yetu. Uchaguzi wa madiwani, wabunge, wawakilishi na rais. Litakuwa jambo jema kama tutawachagua viongizi bora watakaotuongiza pale walipoishia wengine. Nawataki heri na Baraka nyingi. Tukutane 25/10/2015.

Ramani mpya ya mji wa Kusulu

Hii ni ramani mpya ya mji wa Kasulu, mkoni Kigoma baada ya kuwa halmashauri ya mji.
Chanzo: Leonard Kilamuhama / Kigoma Networking Group

Ladha mpya katika filamu Tanzania,,,

Pichani ni bbaadahi ya wasanii walioigiza Filamu ya THE STOLEN DREAM, iliyotengenezwa na kampuni ya THE ICON ENTERTIMENT chini ya producer ni FETTY KABOMA.
Baadhi ya mastar waliomo ni chuchu hans,jengua,danny kaboma (msanii wa zamani wa kundi la kidedea),anna msangi au siri (mama anaefanya vizuri sokoni akiwa na filamu kibao kama ndoa yangu ya kanumba aliyocheza kama mama wa jack worlper na nyingine nyingi),bi ndoza au bi farida anaecheza kwenye tamthia ya siri ya mtungi na wengine wengi.
Director wa filamu hiyo ni ABUBAKARI MTEGWA,,

Swahili Abroad,

Blog kabambe na ya ukweli wa news za kijanja kuhusu pilikapilika za maisha ya ughaibuni wanayoishi ndugu zetu watokeao Afrika Mashariki, itakuwa hewani muda wowote kuanzia leo. Maudhui makuu ya blog hii ni kuwa daraja la habari za  maisha halisi kati ya ughaibuni na Afrika Mashariki. Wanaafrika Mashariki wanaozungumza lugha ya Kiswahili walio ughaibuni, wanahusika pia. Hapa utapata makala zinazozungumzia maisha yao halisi, burudani, michezo, harakati za kimaisha, masomo, kazi, ubunifu, urembo pamoja na mengine mengi yanayowazunguka. Yeyote anayefanya mazuri kuhusu lugha hii, utamkuta hapa. Kwa lugha nyepesi tunaweza kusema, "hii ndio nyumba ya Kiswahili Ulimwenguni!" Jaribu leo kufungua www.swahiliabroad.blogspot.com

Mwakilishi wa Tanzania, Big Brother Africa 2013 atajwa.

 Mwakilishi wa Tanzania katika shindano la Big Brother Africa 2013, ni Mwanamuziki Feza Kessy (pichani) ambaye ni mwenyeji wa Arusha. Feza mwenye umri wa miaka 25 ana elimu ya Cheti katika Teknolojia ya Habari (IT).

Obama afunga hotel, Dar

Wakati Rais wa Marekani, Barrack Obama akitarajiwa kuwasili na msafara wa watu 700, baadhi ya hoteli zenye hadhi ya nyota tano jijini Dar es Salaam zimeanza kusitisha kupokea wageni kutokana na ujio huo.
Taarifa iliyotolewa na Ubalozi wa Marekani ilisema Rais huyo, anatarajiwa kuwasili nchini Julai Mosi kwa ajili ya ziara ya siku tatu hadi Julai 3 mwaka huu ili kuimarisha uhusiano baina ya nchi hiyo pamoja na nchi za Afrika. Msafara huo utajumuisha watu mbalimbali wakiwamo wafanyabiashara.

"Nilimsaidia Kikwete uchaguzi wa 2010" Lipumba

MWENYEKITI wa Chama cha Wananchi (CUF), Profesa Ibrahim Lipumba, ameibua suala zito akikihusisha chama chake na “kumnusuru” Rais Jakaya Kikwete katika uchaguzi mkuu uliopita.
Profesa Lipumba alitoboa siri hiyo katika Msikiti wa Idrissa, Kariakoo, jijini Dar es Salaam, alikokwenda kuswali swala ya Ijumaa.
Huku akisisitiza juu ya umuhimu wa mshikamano wa kiimani, Profesa Lipumba alianza kwa kuzungumzia matokeo ya uchaguzi mkuu wa 2010, na ushindani mkali wa kisiasa uliokuwapo.
Alisema hawaoni matunda ya jitihada walizofanya kumnusuru Rais Kikwete asishindwe, kwani hata chini ya uongozi wake, Waislamu wameendelea kutothaminiwa.
“Ninyi masheikh mnajua vizuri zaidi hali ya kisiasa ilivyokuwa, kwamba ilibidi zifanyike juhudi za makusudi ili kuokoa jahazi. Lakini pamoja na kuliokoa jahazi, hali halisi inaonyesha mpaka sasa hakuna matunda yoyote yaliyopatikana, na tupo katika mtihani mgumu zaidi,” alisema.
Katika hali ambayo inasemekana ushindi wa Rais Kikwete ulipatikana kwa mbinu, huku wengine wakiituhumu Tume ya Taifa ya Uchaguzi kuwa ilimnusuru mgombea wa CCM, kauli hii ya Profesa Lipumba inadokeza kwamba anajua mkakati zaidi wa kazi ya Tume ya Uchaguzi.
Katika hali isiyo ya kawaida, Profesa Lipumba anaonekana kuhamasisha Waislamu kujipanga akisema “wenzetu wameanza kujipanga” kuelekea 2015.

“Kwahiyo kama Waislamu tunataka kupata haki zetu, kama tunataka kuishi kama raia wa daraja la kwanza katika nchi yetu, lazima tujipange kuelekea uchaguzi mkuu wa 2015; na sisi tuanze kujipanga kwa sababu wenzetu wameanza kujipanga, vinginevyo tutaendelea kubaki maskini na raia wa daraja la nne katika nchi yetu wenyewe.
“Mwaka 2010 wakati mshindi wa uchaguzi wa rais alipotangazwa, mimi nilikwenda kwenye hafla ya kutangazwa matokeo, na nilikwenda makusudi tu, siyo kwamba uchaguzi ulikuwa huru na wa haki, ila nilikwenda makusudi kwa kujua hali ya kisiasa ilivyokuwa wakati huo.
“Huku nilikutana na Sheikh Basaleh. Nilipokutana naye, alinipongeza; sijui kama yeye anakumbuka, akaniambia ‘umeweka mbele imani yako na umekuwa mwelewa wa mambo.’”
Hata hivyo, licha ya Profesa Lipumba kuwaambia Waislamu wajipange kwa ajili ya uchaguzi mkuu, hakusema wajipange kupitia chama kipi.
Lakini alisisitiza kwamba uchaguzi ujao ni zaidi ya siasa au rais yupi anafaa, bali maslahi, hasa ya rasilimali nyeti zinazopatikana katika ukanda wa Pwani ya Mashariki, eneo ambalo alisema linakaliwa zaidi na watu wenye imani ya Kiislamu.
Katika moja ya kauli zake, Profesa Lipumba alisema kwamba kuna chama kimoja kinataka kuchukua madaraka ya nchi, lakini kinasaidiwa na mataifa ya magharibi, yasiyoenzi wala kuthamini imani ya Kiislamu.

Kwa muda sasa, zimekuwapo tetesi kwamba CCM imekuwa inafanya siasa za udini dhidi ya vyama vya upinzani, hasa inapoona maslahi yake yapo hatarini.
Mwaka 2010 makada kadhaa wa CCM walitumia mitandao ya simu kuchonga (spoofing) ujumbe wa simu ulioshambulia mgombea mmoja wa upinzani, ukimhusisha na imani yake.
Kauli ya Lipumba imethibitisha pia minong’ono iliyokuwapo muda mrefu kuwa baadhi ya kura za Profesa Lipumba zilipotelea kwa Rais Kikwete.
Katika uchaguzi huo, Lipumba alitangazwa kushika namba ya tatu, nyuma ya Rais Kikwete na Dk. Willibrod Slaa wa CHADEMA.
Alipoulizwa kuhusu ziara yake msikitini na kauli aliyotoa, Profesa Lipumba alikiri kwamba alikwenda kuzungumzia hali ya kisiasa nchini.

Rama mla watu, yuko huru

[ GUSHIT NEWZZZZZZZZZZZZZ....!!! ]

RAMA MLA WATU AACHIWA HURU

Mahakama kuu kanda ya Dar es Salaam imeamua kumuachia huru Ramadhani Selemani Mussa ambaye alikuwa akikabiliwa na kesi ya kukutwa na kichwa cha mtu. Rama, ambaye muda wote huo alikuwa rumande gereza la Segerea akisota kusubiri hukumu yake, alikamatwa hospitali ya Muhimbili mwaka 2008 ambapo pia alikiri kuwa alikuwa na tabia ya kula nyama za watu ambayo amefundishwa kichawi toka alipokuwa mdogo.

 Mahakama imemuachia huru kwasababu mtuhumiwa alitenda kosa hilo pasipo kuwa na akili timamu. Hata hivyo mahakama hiyo imetoa agizo la kuendelea kumuweka kijana huyo katika hospitali ya wagonjwa wenye matatizo ya akili, hospitali ya Isanga iliyopo Dodoma mpaka pale atakapona ndipo aruhusiwe kurudi mtaaani.habari kutoka karibu ndani
Mahakama kuu kanda ya Dar es Salaam imeamua kumuachia huru Ramadhani Selemani Mussa ambaye alikuwa akikabiliwa na kesi ya kukutwa na kichwa cha mtu. Rama, ambaye muda wote huo alikuwa rumande gereza la Segerea akisota kusubiri hukumu yake, alikamatwa hospitali ya Muhimbili mwaka 2008 ambapo pia alikiri kuwa alikuwa na tabia ya kula nyama za watu ambayo amefundishwa kichawi toka alipokuwa mdogo.
Mahakama imemuachia huru kwa sababu mtuhumiwa alitenda kosa hilo pasipo kuwa na akili timamu. Hata hivyo mahakama hiyo imetoa agizo la kuendelea kumuweka kijana huyo katika hospitali ya wagonjwa wenye matatizo ya akili, hospitali ya Isanga iliyopo Dodoma mpaka pale atakapopona ndipo aruhusiwe kurudi mtaaani.

M23 wamwogopa Ban Ki Moon!

Goma DRC

Katibu mkuu wa UN BAN-KI-MOON akitemblea Mji wa Goma huko mashariki mwa DRC akishindikizwa na kiongozi wa Benki ya Dunia

viongozi hao wametembelea Mji wa GOMA huku kukiwa na hali ya wasiwasi kufatia mapigano ineyoendelea pembezoni mw Mji huo huku waasi wa M23 wakitwangana na jeshi la serikali ya Congo FRDC .Laki hata hivyo leo hakukusikika mlio wa risasi tangu asubui waasi wa M23 wakisema viongozi hao wapashwa kuheshimiwa na kuwapa muda wakujua picha kamili ya hali ya mambo na chanzo cha mzozo mashariki mwa DRC.

HAPO wako naye Gavana wa JULIEN PALUKU wa Kivu kaskazini wakitoka kwenye uwanja wandege ulieko karibu na mpaka wa Rwanda na DRC.

PICA tumepata kutoka MUSTAFA KEMAL mfanya kazi kunako ofisi ya Gavana Kivu kaskazini.
Katibu mkuu wa UN BAN-KI-MOON akitemblea Mji wa Goma
 huko mashariki mwa DRC akishindikizwa na kiongozi wa Benki ya Dunia.

 Viongozi hao wametembelea Mji wa GOMA huku kukiwa na hali ya wasiwasi kufuatia mapigano yanayoendelea katika mji huo, huku waasi wa M23 wakitwangana na jeshi la serikali ya Congo FRDC. Lakini hata hivyo leo hakukusikika mlio wa risasi tangu asubuhi, Waasi wa M23 walisema viongozi hao wapaswa kuheshimiwa na kuwapa muda wakujua picha kamili ya hali ya mambo na chanzo cha mzozo mashariki mwa DRC.

Nimezaa na Kanumba

5SELEKT (9:00 Alasiri): Moja.. Mbili... Tatu... Mguu Pande! Make sure haukosi SURPRISE video ya leo.. Tuko na Trailer la .......!! *Jipange*

CHEMBA TOPIC: Kwa nini vijana wengi wanapenda habari za udaku kulio habari za msingi?

Tuko na Manyoka mjengoni, so, fanya kama unadondosha zile COMMENTS hapa kwa wingi, kuanzia time hii!!

#TeamMastaa LEGGOO!!

Polisi watumia vitisho kudai rushwa!

JESHI la Polisi mkoani Morogoro limeingia kwenye kashfa nzito baada ya askari wake watatu na raia wanne kukamatwa wakiwa na kichwa cha binadamu. Tukio hilo lilitokea Mei 7 mwaka huu katika eneo la Mgudeni- Dumila wilayani Kilosa.
Inaelezwa kuwa polisi hao kwa kushirikiana na raia hao walikwenda nyumbani kwa mfanyabiashara Samson Mura na kutaka kumbambikizia kesi ya mauaji.
Mbali ya kubambikizia kesi hiyo, polisi hao wanadaiwa kuomba wapewe Sh milioni 25 na mfanyabiashara huyo ili wasimpeleke kituoni.

Bunge laahirishwa tena leo

BUNGE LAAHIRISHWA TENA LEO:Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh.Anna Makinda ameliahirisha tena bunge leo asubuhi ili kupisha kamati ya uongozi ya Bunge iendelee kukutana ili kutoa maamuzi na tamko kuhusu vurugu za Mtwara zilizojotokeza jana na kusababisha mtu mmoja kufariki dunia na uharibifu mbalimbali kutokea ikiwemo kuchomwa moto nyumba za viongozi wa serikali,chama cha mapinduzi na nyumba ya mwandishi wa habari wa TBC.
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh.Anna Makinda ameliahirisha tena bunge leo asubuhi ili kupisha kamati ya uongozi ya Bunge iendelee kukutana ili kutoa maamuzi na tamko kuhusu vurugu za Mtwara zilizojotokeza jana na kusababisha mtu mmoja kufariki dunia na uharibifu mbalimbali kutokea ikiwemo kuchomwa moto nyumba za viongozi wa serikali,chama cha mapinduzi na nyumba ya mwandishi wa habari wa TBC.

Sheha Zanzibar, amwagiwa tindikali

Sheha wa Tumondo Mohamed Omary Said, amemwagiwa tindikali na mtu asiyejulikana na hivyo kupata maumivu makali sehemu yake ya kifua na jicho kuumia pia.
Sheha huyo alikimbizwa katika Hospitali ya Mnazi mmoja mjini Unguja ambapo alipatiwa matibabu ya dharura.
Kamanda wa polisi wa Mkoa wa Mjini Magharibi, Mukhadam Khamis, amesema chombo kilichotumika kummwagia tindikali Sheha huyo kilipatikana eneo la tukio na kwamba polisi imekichukua kwa kukichunguza kitaalam ili kugundua aliyekuwa akikitumia kwa kuangalia alama za vidole.
Sheha huyo alimwagiwa tindikali jana usiku wakati alipotoka nje ya nyumba yake kuchota maji na ndipo mhalifu huyo alipomwagia tindikali na kwamba hakuweza kumtambua.
Sheha wa Tumondo Mohamed Omary Said akiwa hospitali
 

Mtazamo wangu kuhusu vurugu za Mtwara


Moja ya picha ikionesha moto mjini Mtwara, jana.(chini ni picha ya muasisi wa Taifa letu Hayati mwl. Julius Kambarage Nyerere, mzalendo wa kweli.)


 Chanzo cha vurugu:
Vurugu hizo zilitokana na hatua ya Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo kusisitiza kuwa bomba la gesi kutoka Mtwara na kuja Dar es Salaam litajengwa, jambo lingine linalodaiwa kusababisha ghasia hizo ni hatua ya Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) kutokurusha moja kwa moja matangazo ya Bunge hivyo kuwakosesha wananchi fursa ya kusikiliza bajeti hiyo.
Pia vurugu hizo zilichangiwa na vipeperushi vilivyosambazwa na watu wasiojulikana wakitaka watu kuacha kufanya shughuli zozote na kukaa nyumbani ili kufahamu hatima ya mradi wa usafirishaji wa gesi kutoka Msimbati hadi Dar es Salaam kwa njia ya bomba.                                    
 Athari zilizotokea:
Waandishi wa TBC walitishiwa uhai wa maisha na mali zao. Nyumba na gari la mwandishi, Kassimu Mikongoro, vikachomwa moto na kuteketea kabisa. Pia nyumba za Mbunge wa Mtwara Mjini (CCM), Hasnein Murji na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Tamisemi) ambaye pia ni Mbunge wa Mtwara Vijijini, Hawa Ghasia zilichomwa moto.
Katika Mtaa wa Majengo, kundi la vijana lilivamia Ofisi ya CCM Kata na Ofisi ya Serikali ya Kata na kuanza kuzibomoa. Pia nyumba ya Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Mtwara-Mikindani, Ali Chinkawene ilirushiwa mawe.
Ofisi ya Mtendaji Mtaa wa Msikitini, Kata ya Reli na Ofisi ya CCM Chikongola nazo zimeteketezwa kwa moto. Wanafunzi wa Shule za Msingi Shangani na Majengo walirejeshwa nyumbani baada ya mabomu ya machozi kurindima kuanzia asubuhi hadi mchana.
Mashuhuda wanasema mtu mmoja anaaminika kufariki dunia na wengine kadhaa kujeruhiwa huku askari wanne wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), nao pia wakipoteza maisha katika ajali wakitokea Nachingwea kwenda Mtwara ili kusaidia kutuliza vurugu hizo. Katika ajali hiyo, askari 20 walijeruhiwa, wengi wao vibaya na saba walinusurika.
Tangu asubuhi kama ilivyokuwa Mei, 17 mwaka huu, Mji wa Mtwara ulikuwa kimya na huduma nyingi za kijamii zilisimama ikiwamo usafiri wa pikipiki, daladala, mabasi maduka na masoko.
Milio ya risasi na mabomu kama vitani:
Milio ya risasi za moto na mabomu ya machozi vilisikika kila kona na hasa Mitaa ya Mdenga, Magomeni na Shengena Mjini Mtwara ambako hali ilikuwa mbaya kutokana na kuwapo kwa mapambano kati ya polisi na vijana.
Turejee mifano:Rwanda:
Wakoloni Wabelgiji, waliikatakata nchi ya Rwanda katika makundi mawili, kutokana na mfumo wao wa utawala ili kujinufaisha na madini yanayopatikana magharibi ya nchi hiyo. Mfumo huo uliwakandamiza kimakabila, kabila la Watusti wakakwezwa na Wahutu wakashushwa kubakia wafanyakazi hasa mashambani wakati Watusti walikuwa wafanyakzi maofisini. Watusi na Wahutu, ni makabila  makubwa nchini Rwanda. Wabelgiji walipoondoka kurudi Ulaya, Wahutu, wakapata nafasi ya kujitetea. Njia waliyotumia kutafuta haki ikawa vita. Mwaka 1994, ikazuka vita mbaya kuwahi utokotokea hapa Afrika Mashariki. Watu zaidi ya milioni moja waliuawa katika vita hiyo.
Rwanda ya leo:
Kwa sasa nchi hiyo, iko katika ramani ya moja ya nchi zenye uchumi mzuri katika Afrika Mashariki, sharia ya kukomesha ubunafsi wa tabaka za ukabila, inasimamiwa vilivyo. Ni kosa la jinai, kutaja kabila la mhutu au mtusi kuonesha tofauti zao. Vitambulisho vya utaifa vimendikwa Mnyarwanda, na sio Mhutu, Mtutsi wala Mtwa.
Mtazamo na maoni yangu:
Napozitazama vurugu hizi, Napata mawazo ya mbali sana kuhusu matokeo ya vurugu! Najiuliza swali moja kuu, kwamba, matokeo ya vurugu nini? Kama chanzo ni gesi hii isisafirishwe kuja jijini Dar es salaam, je huo sio ubinafsi?
Bila shaka ubinafsi wa aina hii katika nchi yetu ukiachwa uendelee, utapoteza maana halisi ya umoja wa kitaifa. Nasema hivyo kwa kumaanisha kuwa, kila mkoa unaweza kudai mali asili inayopatikana katika mkoa wake, iwe ni mali ya mkoa husika, jambo ambalo haliwezekani kabisa katika nchi yenye umoja  uliotokana na ujamaa.
Wanasisa na wanaojiita wanaharakati, wadhibitiwe na kuadhibiwa pale watakathibitika kuhusika kwa njia moja au nyingine.
Binafsi, nitaendelea kuwalalamikia pia wakoloni. Sasa wanajifanya wataalamu na watoa misaada. Hawa, ndio wanaoleta chokochoko hizi. Sisi tupigane kwa kuonana wabaya ili wanufaike wao. Imani yangu inanituma huko kwa kuwa nikirudi katika historia ya vita nyingi zinazotokea katika bara la Afrika na mashariki ya kati, wazungu hawa, wanakuwa mstari wa mbele kukimbilia kutoa misaada ya kibinadamu. Kutoa kwao misaada, sikatai, ila wanaingiza faida kubwa sana nyuma ya vita wanazozitengeneza wao.
Wanauza silaha, maana nchi hizi hazina uwezo kiviwanda kuzalisha silaha!
Wanapora rasilimali muhimu na kuondoka nazo makwao.
Vurugu hizi za Mtwara, zina mikono ya watu wenye pesa na tamaa ya kujinufaisha wenyewe na familia zao.
Chokochoko za uvunjifu wa amani ya nchi yetu, zimeanzia mbali hadi kufikia Mtwara. Udini unaosmabaa chini kwa chini pamoja na ukabila.
Kwa hili srikali ikae chini na wananchi wa Mtwara, kuwaelewesha upya faida watakazopata juu ya ugunduzi huu wa gesi na iwe wazi kwao.
Wananchi pia waiheshimu serikali na kuwapuuza wachochezi hawa wenye nia mbaya na amani ya nchi yetu.
Waandishi na vyombo vya habari, wawe mstari wa mbele kuripoti kwa uweledi wa kizalendo habari zote zinazohusu Mtwara na gesi. Zisiandikwe au kutangazwa habari zenye uchochezi au zeney kuleta sintofahamu yoyote.

Bandari ya Dar es Salaam,hasara kwa Taifa.

EAST AFRICA BREAKFAST..(12 Asubuhi) Ripoti ya Benki Dunia iliyotoka jana imesema Tanzania inapoteza ya dola za kimarekani bilioni 1.8 (Trilioni 2.9) kutokana na ukosefu wa ufanisi katika Bandari ya Dar-es-salaam...nini maoni yako?
Ripoti ya Benki ya Dunia iliyotoka jana imesema Tanzania inapoteza ya dola za kimarekani bilioni 1.8 (Trilioni 2.9) kutokana na ukosefu wa ufanisi katika Bandari ya Dar-es-salaam.

Mamia waikimbia Congo.


Mamia wanatoroka maeneo ya vita Goma
kukimbilia usalama wao.

Fundisha Kiswahili Marekani.

Fulbright Foreign Language Teaching Assistant Program

Are you Eligible?
You must meet the following minimum eligibility requirements in order to apply for this program for the 2013-2014 cycle (now open):
 • Be an English Teacher
 • Be between 21-29 years old
 • Earn a Bachelor’s degree by June 2012
 • Have excellent English communication skills
 • Speak fluent Kiswahili
 • Have excellent academic track record
 • Be able to discuss and showcase Tanzanian culture
 • Be willing to travel without your family for one academic year
 • Be willing to teach Kiswahili at U.S. institutions
 • Be able to work independently as well as part of a team
Kama una vigezo hivyo, unaweza kuendelea kwa kugonga hapa.
 Usichelewe.

Prof. Jay awa mwanachama wa Chadema, rasmi.

Prof. Jay akikabidhiwa kadi Mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi
Prof. Jay akikabidhiwa kadi na Mbunge wa
Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi

Msanii maarufu wa muziki wa kizazi kipya nchini, Joseph Haule,"Prof. Jay), ametangaza rasmi kujiunga na chama kikubwa cha upinzani nchini, Chama Cha Deomokrasia na Maendeleo (CHADEMA.).
Alitoa kauli hiyo jana mjini Dodoma alipokwenda kuhudhuria moja ya vikao vya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, vinavyoendela mjini humo.

Kamanda wa polisi atajwa, kifo cha kamanda Barlow, Mwanza.

Taarifa zilizozagaa hivi sasa katika mitandao zinadai kuwa
aliyekuwa kamanda wa Jeshi la Polisi mkoa wa Mwanza ameuawa na genge
ndani ya Polisi akiwemo Kamanda Polisi anayejulikana kwa jina la Muna.
       Katika tovuti ya gazeti la Jamhuri, Deo Balile anaonekana kulalamikia gazeti hilo kununuliwa kwa jumla na watu wasiojulikana.
          Kuvuja kwa siri hiyo kumetokana na mmoja wa jambazi sugu ajulikanaye kwa
jina la Edward Malele kujisalimisha ktk vyombo vya ulinzi na kutoa siri
zote.
Jambazi huyu aliombwa wa genge ndani ya polisi kushiriki katika mpango
wa kumwua kamanda Barlow. Akakataa kwa kuwa aliwahi kumfahamu kwa karibu
kamanda Barlow.
          Baada ya kukataa kutekeleza agizo hilo baada ya siku chache alishtakiwa
kwa kosa la ujambazi na kuswekwa Rumande.
Akiwa huko ndani ya wiki moja alisikia habari za kifo cha kamanda
Barlow. Akajua akina na Muna aliowakatalia wamefanya kazi aliyoikataa
yeye. Na alijua yuko mahabusu kwa sababu ya kukataa mradi huo.
Baada ya kukaa huko muda mrefu bila shitaka kueleweka wala mshataki wake
huko Lupango walimua kumwaichia. Akagoma kutoka kwa sababu anajua kuwa,
kwa kuwa amepelekwa huko ili kuficha siri hivyo, akitoka lazima
atauawa. Baada ya muda akaamua kukubali kutoka lupango na kukimbilia
kituo cha JWTZ huko Mwanza.
         Huko JWTZ Alijieleza vya kutosha na wanajeshi walimwonea huruma wakampa
Tsh 10,000/= ilie aende Bungeni huku wakiwa wamemkabidhi namba za simu
za wabunge 2 wa upinzani ili wamsaidie.
Kutokana na kutokuelewa kwake alipokuwa anashangaa shangaa katika eneo
la Bunge, alikamatwa na polisi wanalinda eneo hilo. Polisi hao wakapiga
simu Dodoma central na Mwanza. Haraka haraka mwanza wakataka arudishwe
mwanza kwa kuwa ni jambazi sugu.
          Hata hivyo, kwa katika kurupushani hiyo taarifa zimeshameshamfikia Pinda
na Nchimbi ambapo gazeti linaripoti kuwa Pinda ameagiza kijana huyo
apewe ulinzi na asirudishwe mwanza.
Tarifa zaidi zinaema kuwa mpaka sasa amepelekwa kusiko julikana.

Jeshi la Nigeria lauwa wanachama wa Boko Haram

Majeshi ya Nigeria yakipiga doriaJeshi la Nigeria linasema limeuwa wanamgambo 14 wa kundi la Boko Haram na kuwakamata wengine 20 Jumapili. Jumanne iliyopita rais wa Nigeria Goodluck Jonathan aliamrisha kupelekwa kwa malefu ya wanajeshi upande wa kaskazini mwa nchi kupambana na wanachama wa Boko Haram,kundi la wanamgambo ambalo linalaumiwa kwa kusababisha vifo vya maelfu ya watu katika muda wa miaka minne iliyopita.
Lakini kufikia Jumapili Jeshi lilisema wanamgambo hao 24 wa Boko Haram walikuwa wameuawa na wengine 85 kukamatwa. Baadhi ya wachambuzi wanahofu kuwa jeshi, ambalo makundi ya kimataifa ya kutetea haki za binadamu yameshtumu kwa mauaji ya kiholela na ukiukwaji mwingine, huenda likatenga watu kwa kuuwa raia pale linapowasaka wanachama wa Boko Haram.

Flaviana Matata na Fastjet katika kumbukumbu ya Mv Bukoba leo, Mwanza

Mwanamitindo wa kimataifa Flaviana Matata na fastjet watakuwa kwenye kumbukumbu ya waliofariki katika ajali ya MV Bukoba Mwanza, leo Jumanne tarehe 21 Mei.

Njoo ujumuike nasi katika kuwakumbuka wale waliopoteza maisha katika ajali hii, kukabiliana na changamoto na kubadilishana mawazo juu ya nini kifanyike katika kuhakikisha usalama wa usafiri wa majini.
Mwanamitindo wa kimataifa Flaviana Matata na fastjet watakuwa kwenye kumbukumbu ya waliofariki katika ajali ya MV Bukoba Mwanza, leo Jumanne tarehe 21 Mei.
 Njoo ujumuike nasi katika kuwakumbuka wale waliopoteza maisha katika ajali hii, kukabiliana na changamoto na kubadilishana mawazo juu ya nini kifanyike katika kuhakikisha usalama wa usafiri wa majini.

Kumbukukumbu ya MV Bukoba

    

Tarehe kama ya leo (Mei 21) mwaka 1996 meli ya MV Bukoba ilizama katika Ziwa Victoria. Usiku wa kuamkia siku ya ajali, meli hiyo ilipakia abiria kati ya 750 na 800 pamoja na wafanyakazi 37. Kati ya hao, 114 waliokolewa wakiwa hai; wakati 391 waliopolewa wakiwa wamefariki na kuzikwa katika makaburi ya Igoma, nje kidogo ya Jiji la Mwanza.
        Miili mingine ilichukuliwa na jamaa kuzikwa kwao. Jumla ya miili 332 haikupatikana. Kila mwaka, ifikapo Mei 21 tunawakumbuka waliopoteza maisha katika ajali hii. MV Bukoba ilijengwa na kampuni ya Kibelgiji na ilizinduliwa 27 Julai 1979. Mungu aendelee kuwalaza mahali pema peponi waliopoteza maisha na kuwafariji waliopotéza maràfiki na wanafamilia.

Kagame akosoa kikosi cha UN DRC

Rwanda imekuwa ikikana mara kwa mara tuhuma
 kuwa inahusika na vita DRC
 
Rais wa Rwanda Paul Kagame alitoa mtazamo mkali wa ujumbe wa kulinda amani wa Umoja wa mataifa ulioko katika Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo.
Kagame ameiambia BBC kwamba kikosi cha Umoja wa Mataifa cha askari elfu 20 kilichopelekwa miaka 14 iliyopita, hakijafanya lolote kutatua chanzo cha matatizo ya Congo na wakati mwingine kimeufanya mzozo huo kuwa mmbaya zaidi.
Amesema visa vya mapigano , ghasia, na watu kupoteza makaazi yao kulitishia usalama wa eneo zima.
Serikali ya rais Kagame imekana mara kwa mara tuhuma za Umoja wa mataifa na makundi ya kutetea haki za binadamu kwamba Rwanda inawasaidia wanamgambo mashariki mwa Congo.
Rais Kagame amesema kuwa kutumia nguvu kungesaidia ikiwa tu inekuwa inalenga kusaidia msimamo fulani wa kisiasa

WAVAMIWA KWA KUMTANGAZA MUSEVENI

 
Polisi nchini Ugandan wamevamia ofisi za magazeti kufuatia taarifa kwamba Rais Yeweri Museveni anamuandaa mwanawe wa kiume kumrithi urais.
Vituo viwili vya Redio pia vamiwa na kuzimwa , hii ni kwa muujibu wa gazeti la serikali la New Vision.
Wiki iliyopita magazeti ya Uganda yalidai kuwa kuna njama za kuwaua wale watakao pinga mpango wa Rais Museveni kumuandaa mwanawe kuchukua madaraka ya Uganda.
Magazeti hayo yalidai kuwa mipango hiyo ya mauaji yalitolewa na Mkuu fulani wa jeshi la Uganda.
Bwana Museveni, ambaye amekuwa madarakani tangu 1986, anatarajiwa kung'atuka uongozini mwaka 2016.
Kwa muda mrefu kumekuwa na madai kwamba Museveni anamuandaa mwanawe Muhoozi Kainerugaba,ambaye ni brigadier jeshini kushikilia uongozi wa Uganda.
Lakini serikali ya Museveni imekanusha kwamba kuna mipango kama hiyo.

Mandhari ya Edo - Kawagoe nchini Japani.

Katika mfululizo wa makala za matembezi, leo tunatembelea nchini Japani.
Matembezi yanajikita katika mitaa ya mji wa Kawagoe inayodumisha mandhari ya Edo katika mkoa wa Saitama, ambapo unaweza kuona majengo mengi yaliyojengwa zaidi ya miaka 100 iliyopita.

Hili ni jengo la Osawa lililojengwa mwaka 1792.
Kwa miaka mingi lilitumika kama duka la viatu,
lakini siku hizi linatumika kuuza bidhaa za sanaa kwa ajili ya watalii.

Majengo mengi ya kuvutia ya mbao yenye ghorofa mbili yenye paa za vigae vyeusi, yamepangana katika mtaa ujulikanao kama Ichibangai-dori, unaoanzia kusini hadi kaskazini mwa mji.

Honmaru Goten, jengo kuu katikati mwa kasri la Kawagoe bado lipo.
Haya ni makazi ambayo mtawala wa eneo hilo alikuwa akifanya kazi na kuishi.


Mto huu ulikuwa ni njia muhimu ya usafiri wa majini kati ya Edo na Kawagoe.
Sehemu hii ilikuwa ni gati kubwa zaidi ya Kawagoe.

Viazi vitamu hulimwa Kawagoe, na kuna aina mbalimbali za viazi vitamu.
Imoyokan, au mgando wa rojo la viazi vitamu, hutengenezwa kwa kuchemsha viazi vitamu kwa mvuke, na baadaye kutengeneza mgando wa rojo hilo katika umbo la mche mstatili.

Makala yetu kwa leo inaishia hapa. Wiki ijayo tutaendelea kutembelea miji kadhaa ya Jani. Kama una maoni au lolote usisite kutuandikia. Pia unaweza kutuandikia ukiomba tutembelee wapi unapopenda wewe. Tukutane tena wiki ijayo,siku kama ya leo.

Jeshi la Congo lashambuliwa na M23, leo.

Jeshi la Congo DRC linasema kuwa leo limeshambuliwa na waasi wa M23 katika kijiji cha Muja na RUSAYO.
Msemaji wa jeshi la Congo Kivu kaskazini OLIVIER AMULI alisema kuwa hadi sasa mapigano yanaendelea katika Mbuga ya wanyama ya pori la Virunga kilometa 15 na Mji wa Goma.

GARI LA AFISA WA POLISI LAKUTWA NA MAGUNIA 18 YA BANGI MOSHI

      SIKU chache baada ya Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam kuwakamata askari 16 wakituhumiwa kujihusisha na biashara ya magendo, askari wengine wawili wa jeshi hilo wamekamatwa mkoani Kilimanjaro wakiwa na shehena kubwa ya bangi wakiisafrisha kwenda nchini Kenya.
      Askari hao walikamatwa Mei 19 mwaka huu saa nne usiku eneo la Himo, Kilemapofu, Wilaya ya Moshi Vijijini wakiwa na magunia 18 ya bangi ambayo walikuwa wameyapakia kwenye gari la Mkuu wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU) mkoani Arusha aina ya Toyota Land Cruiser lenye namba PT 2025.

"ME & MA FUTURE WIFE" - Diamond

#me and my future wife.
Habari kutoka katika ukurasa wake wa facebook, mwanamuziki Nasseb Abdul maarufu kama Diamond Platnamz, zinassomeka kuwa huyo (pichani) ndiye mkewe mtarajiwa.
          Hata hivyo maoni ya wasomaji wake wengi wameonekana kumkandia vilivyo kwa tabia yake ya kumtambulisha kila demu anayekuwa naye kuwa ndiye mkewe mtarajiwa! Watarajiwa wako wangapi?

SOMA NORWAY!

University of Oslo
fUngua University of Oslo

"UDINI UNAOENDELEA NCHINI, UNA MKONO WA NJE! " -RAISI KIKWETE


        Rais Jakaya Kikwete amebainisha kuwa vurugu za kidini na kisiasa zinazotokea nchini, zina uhusiano na watu wa nchi za nje.
      Alitoa kauli hiyo jana kwenye ibada maalumu ya kuwekwa wakfu kwa Askofu Mkuu wa Sitta wa Kanisa Anglikana Tanzania, Dk Jacob Chimeledya.
Rais Kikwete alikuwa mgeni rasmi kwenye ibada hiyo iliyofanyika kwenye Kanisa Kuu la Roho Mtakatifu.
    “Wanaohamasisha vurugu hizo ni watu wenye uhusiano ya karibu na watu wa nje ambao mambo yakiharibika nchini watakuwa wa kwanza kupanda ndege, ilhali wakiendelea kutoa matamko ya uchochezi wakiwa nje ya nchi wakati wengine wakiendelea kuumia,” alisema Kikwete.

IRINGA HAPATOSHI NAKO!

KUTOKA IRINGA: Polisi wapiga mabomu ya machozi na kutawanya machinga. Hii ni kufuatia machinga kurudi kwenye maeneo yaliyokatazwa kufanyia biashara. 

Picha na habari zaidi ---> http://j.mp/15Y7qK0
  Polisi wapiga mabomu ya machozi na kutawanya machinga.
Hii ni kufuatia machinga kurudi kwenye maeneo yaliyokatazwa kufanyia biashara.

USISEME KAVUMBAGU, SEMA.... 
Hadi dakika 90 zinamalizika Yanga ilikuwa inaongoza kwa holi 2 bil majibu kutoka kwa Yanga.
Dakika ya 28 Simba walipata penati, akapiga Mussa Mudde na kukosaDk 27 PENALLLLTTY......! Simba inapata penalti baada ya Cannavaro kumchezea vibaya Mrisho Ngassa.
Didier Kavambagu anaipatia Yanga bao la kuongoza
Dakika ya 63, Hamis Kiiza anaipatia Young Africans bao la pili - Young Africans 2 - Simba SC 0

Jamaa baada ya kumalizika kwa match hii, akakutwa analia maeneo ya Msimbazi..


US PRESIDENT VISIT TO TANZANIA


       President of Tanzania Jakaya Mrisho Kikwete (left) shares
            something with US President Barack Obama
 
 
Reports in the Nigerian press yesterday said President Obama would begin his second tour of Africa at the end of next month with visits to South Africa, Tanzania and Rwanda.
         An information specialist in the embassy’s public affairs section, Ms Halima Mbaruku, said she was not aware of the visit. She said the embassy closes at 11am on Fridays.
       “President Barack Obama of the United States is billed to begin his second tour of Africa at the end of June with visits to South Africa, Tanzania and Rwanda,” the influential News Day reported yesterday. “He will, however, make a stop-over in Nigeria, during which he will hold bilateral discussions with President Goodluck Jonathan and other top government officials.”
       President Barack Obama’s trip to Africa next month may include Tanzania, but the government said yesterday that it has not been officially informed of the visit.
Foreign and International Cooperation minister Bernard Membe said they were aware of the US president’s tour but they had not been informed of his coming here.

          “We are waiting for official confirmation on the visit,” he told The Citizen on Saturday in a text message.
          In February 2008, Tanzania hosted his predecessor, Mr George W. Bush, who also visited Rwanda. Highlights of the successful state visit included signing of a $698 million grant under the Millennium Challenge Account arrangement.

        Mid-last month, US Secretary of State John Kerry told a US congressional committee that President Barack Obama “will travel” to Africa. He offered no details regarding the timing and itinerary of the trip.

     The visit comes amid growing concern in Washington about China’s role in sub-Saharan Africa, with pressure mounting for President Obama to pay more direct attention to the continent. As was the case in 2009, Mr Obama is unlikely to visit Kenya, where his father was born.

     Africa specialists in the US say a visit to East Africa’s largest economy would not be possible as long as President Uhuru Kenyatta remains under indictment by the International Criminal Court.

MAAFA BAHARI YA HINDI

Watu watatu wakaazi wa Zanzibar wamepotea baharini baada ya boti yao waliokuwa wakitumia kwa ajili ya kazi ya kusafirisha mafuta ya magendo kupotea au kuzama katika bahari ya Hindi.

TAMKO LA JIDE WAKATI WA KESI YAKE NA JOE NA RUGE.


Nadhani baada ya hii, maswali yatapungua kama sio kuisha kabisa...Nafahamu kila mtu anasoma kwa wakati wake pengine hamkuona sababu nilizoelezea kwanini sijatoa waraka mwingine Tar 15 kama nilivyo ahidi.
       Sababu ni kuwa mahakama imesema nisizungumzie hilo swala kwasasa, ambapo kesi bado iko mahakamani...Mpaka nitakapopewa ruhusa ya kuzungumza au kutozungumza tena

NIGERIA BADO HALI SI SHWARI!


Vita vyashika kasi dhidi ya Boko Haram hali iliyoilazimu serikali kutoa amri ya kutotoka nje usiku katika jimbo la Adamawa nchini Nigeria.Jimbo hilo limeungana na mengine mawili ya kaskazini mashariki ya, Borno na Yobe, ambako serikali inasema kuwa wanajeshi wameanza oparesheni kubwa dhidi ya wapiganaji wa kiislamu wa kundi la Boko Haram .

ALICHOANDIKA ZITTO KABWE KUHUSU USAFIRI WA RELI DAR

     Ubinafsishaji wa usafiri wa reli Dar Es salaam - uk. 24 wa hotuba ya Waziri Mwakyembe " .... Wizara kupitia RAHCO itakamilisha mchakato wa kumpata mwekezaji na mwendeshaji wa huduma ya usafiri wa treni ya abiria katika jiji la Dar Es Salaam atakayetumia miundombinu ya reli iliyopo....."
      Kwa nini serikali haikuanza Kwa kuwa na Shirika la Reli Dar Es Salaam kabla ya kwenda kwenye ubinafsishaji? Tumeshafanya tathmini ya ubinafsishaji wa awali wa usafiri wa reli nchini? Tumejifunza nini?

TAZAMA HII!

!!!!!!!!!!!

GESI YA TANZANIA

Serikali imeshauriwa kuongeza juhudi za utoaji wa taarifa za rasimali za gesi na nishati mbalimbali kwa wananchi, baada ya Tanzania kushika nafasi ya 27 kati ya nchi 58 za Africa katika usimamizi na utawala wa rasilimali hizo katika ripoti iliyotolewa na taasisi ya utafiti ya Revenue watch

GHOROFA LAUA TENA DAR!

Gorofa linalojengwa katika eneo la Ilala Bungoni mtaa wa mafuriko jijini Dar es salaam bila kufuata sheria ya kuweka vizuizi kwa ajili ya usalama wa watu,imesababisha kifo cha mwanafunzi wa darasa la kwanza mwenye umri wa miaka 6 baada ya kupigwa na mbao yenye misumari iliyorushwa kutoka juu ya gorofa hilo na kufariki papo hapo.

AGNESS MASOGANGE:SIKWENDA SAUZI KUJIUZA!


VIDEO Queen wa Bongo, Agness Gerald ‘Masogange’ (pichani) ameibuka na kusema kuwa hakwenda Afrika ya Kusini ‘Sauz’ kujiuza kama baadhi ya watu walivyompakazia
Akipiga stori na zaidi, Masogange ambaye iliwahi kuvuja video yake ya utupu mwaka jana, alifafanua kuwa picha mpya zinazodaiwa kuwa ni za nusu utupu zilizozagaa mtandaoni, zilisababishwa na ulevi na si kweli kwamba ni za kujiuza.

HATARIIIIIIIIII........NIGERIA!

Raisi wa Nigeria Goodluck Jonathan ametangaza hali ya hatari baada ya kutokea milipuko mitatu kwenye miji tofauti ya nchi hiyo.

Kwenye hoja yake anazilaumu jeshi haramu za kiislamu kwa milipuko hiyo ambayo imekuwa ikitokea kuanzia mwaka 2010.
      Raisi wa Nigeria Goodluck Jonathan ametangaza hali ya hatari baada ya kutokea milipuko mitatu kwenye miji tofauti ya nchi hiyo.
        Kwenye hoja yake anazilaumu jeshi haramu za kiislamu kwa milipuko hiyo ambayo imekuwa ikitokea kuanzia mwaka 2010.

DRC VITANI


     Watu zaidi ya 33 wakiwemo wapiganaji Mayi Mayi 22 na askari tiifu kwa serikali 9 wamekufa katika mapigano makali yaliyo jitukiza huko Beni Kivu kaskazini ikiwa ni mashariki mwa Congo kilometa 80 na mpaka wa Uganda.
       Tangu saa kumi za asubuhi wapiganaji Mayi Mayi waingia katika Mji wa Beni hasa kunako jeslo Moja la Mji huo la OZACAF na kuanza kupambana na jeshi la serikali ya Congo.
      Mashiriki ya kiraia katika Muji huo imethibitisaha habari hizo nakusema kua kuna vile raia wengi walio pata majiraha ya risasi na kwa sasa wako hospitali.

JIDE VS KUSAGA...


MWANAMUZIKI Judith Wambura ‘Lady Jaydee’, juzi Jumatatu hatimaye yalimkuta baada ya kuibua simanzi nzito katika Mahakama ya Wilaya ya Kinondoni, Dar, alipofikishwa baada ya kufunguliwa kesi ya madai namba 29/2013 na mabosi wa Clouds Media Group, Ruge Mutahaba na Joseph Kusaga.
         Hali katika mahakama hiyo iligubikwa na huzuni baada ya watu kumuona Lady Jaydee akiwasili eneo hilo sambamba na mumewe Gadner G Habash ambapo walifananishwa na wanandoa mastaa wa Marekani, Shawn Carter ‘Jay Z’ na Beyonce Giselle Knowles, walipotimba mishale ya saa 6:00 mchana.
Risasi Mchanganyiko liliwashuhudia mastaa hao wakiingia eneo hilo huku wakiwekewa ulinzi mkali kama ilivyo kawaida mahakamani kuhakikisha usalama wa watu.
Wawili hao waliongozana hadi chumba cha makarani ambapo walielezwa kesi inayomkabili mwanamuziki huyo na kupangiwa siku ya kesi ambayo ni Mei 27, mwaka huu.
Pia walitajiwa hakimu atakayeendesha kesi yao kuwa ni Athumani Nyamrani wa chumba namba 2 cha mahakama hiyo.
Baada ya kupewa utaratibu wa kesi hiyo walichomoka mahakamani na ndipo wakakutana na paparazi wetu aliyewasimamisha na kutaka kujua madai yaliyofunguliwa.
           JAYDEE AAHIDI KUPAMBANA
Akizungumza na paparazi wetu, Lady Jaydee alisema: “Kesi inahusiana na masuala ya kimtandao, eti Ruge na Kusaga wanadai nimewachafua.
“Kwa leo sitaki kusema mengi, baada ya kupata fomu hizi sasa hivi tunampelekea mwanasheria wetu lakini kila kitu kitawekwa bayana Mei 27, kesi itakapotajwa mbele ya hakimu.
“Kama wameamua kupambana na mimi nitapambana kwa msaada wa Mungu.”
                    HOFU YA KUFILISIWA
Baadhi ya watu waliokuwa mahakamani hapo walionekana kumuonea huruma mwanamuziki huyo kwa jinsi alivyokuwa akihenya kwenye viunga vya mahakama hiyo huku akipishana na askari wenye silaha nzito.
                 Mmoja wa mashuhuda wa tukio hilo alisikika akisema kesi hiyo inaweza kumpotezea muda mwingi na kumuathiri kisaikolojia kwani haijulikani hatima yake ni nini.

                                ADAM NDITI
 Born on 18 September 1994 in Zanzibar, Tanzania, Adam arrived at Chelsea as an Under-13 and can play either left-back or left-wing. It was the more defensive of those roles he filled as the FA Youth Cup was captured in 2012. He was joint-highest youth league appearance maker and played four games for the reserves in 2011/12, his first full-time season which led to a professional contract.
As a schoolboy he amassed 27 youth team appearances, and featured regularly during the 2011 FA Youth Cup run to the semi-final.
... Very quick, he bases his game on Ashley Cole, and enjoys taking players on.
In 2011/12, Nditi was a regular in the side as our youngsters lifted the FA Youth Cup.
This season, once again he's been heavily involved, playing regularly for the Under-21s, while also featuring in both the NextGen Series and FA Youth Cup campaigns.
His versatility means he can play either at left-back or in a more advanced position, which he has done this season, although he has only recently returned from injury.

SHOPS IN GERMANY...

Organic produce is a given in a lot of shops in Germany. But while demand is increasing, cultivation is lagging behind. Since Germany is failing to turn out enough organic products on its own, many of the products must be imported. Do you base your decision to buy food on whether it's organic or not? Or is the price more important? (csc) http://dw.de/p/18XPc
Organic produce is a given in a lot of shops in Germany. But while demand is increasing, cultivation is lagging behind. Since Germany is failing to turn out enough organic products on its own, many of the products must be imported. Do you base your decision to buy food on whether it's organic or not? Or is the price more important? (csc) http://dw.de/p/18XPc

ZITTO KABWE ON TALK.

"Waziri wa Viwanda na Biashara ameagiza mabadiliko ya kanuni katika Sheria ya Hakimiliki ili kuhakikisha kwamba Wasanii wa muziki hapa nchini wanapata mapato stahiki katika biashara ya #RBT . Mirahaba katika biashara ya miito ya simu na matangazo ya televisheni na radio Ni mapato muhimu sana Kwa wasanii. Angalau sasa tunaona Mwanga. Tutaendelea kuishinikiza serikali kulinda wasanii na Hakimiliki zao." amesam Zitto Kabwe katika ukurasa wake wa facebook, muda mfupi uliopita.

The Goodlyfe Crew Moze Radio na Weasel TV on BET tuzo 2013.

Habari mpya na za kufurahisha ni kuwa wanakundi wa The Goodlyfe Crew Moze Radio na Weasel TV kutoka Uganda wamechaguliwa kuingia kwenye kinyang'anyiro cha tuzo ya "Best International Act-Africa" mwaka huu kwenye Black Entertainment Television (BET) Awards 2013. Tamasha la kutoa tuzo hizo litafanyika Nokia Theatre mji wa Los Angeles June 30, 2013.
Wanakundi wa The Goodlyfe Crew Moze Radio na Weasel TV kutoka Uganda wamechaguliwa kuingia kwenye kinyang'anyiro cha tuzo ya "Best International Act-Africa" mwaka huu kwenye Black Entertainment Television (BET) Awards 2013. Tamasha la kutoa tuzo hizo litafanyika Nokia Theatre mji wa Los Angeles June 30, 2013.

MICROSOFT:

Today, as part of our 4Afrika Initiative, we’re excited to announce another TV white spaces project – this time in Tanzania. We’re partnering with the Tanzania Commission for Science and Technology (COSTECH) and local internet service provider, UhuruOne, to provide affordable wireless broadband access to university students and faculty in Dar es Salaam. http://bit.ly/YEAcMf
Today, as part of our 4Afrika Initiative, we’re excited to announce another TV white spaces project – this time in Tanzania. We’re partnering with the Tanzania Commission for Science and Technology (COSTECH) and local internet service provider, UhuruOne, to provide affordable wireless broadband access to university students and faculty in Dar es Salaam.

M23 JISALIMISHENI...

DRC 

SERIKALI YA CONGO IMEOMBA WAASI WA M23 KUJISALIMISHA KWA HARA KABLA HAWASHUGHULIKIWA NA JESHI LA UN MONUSCO HUKO DRC.
WAKATI HUOHUO MABALOZI 15 KUTOKA UMOJA WA AFRIKA UKIONGOZWA NA DR JORAM MUKAMA BISWARO UMETEMBELEA HUKO MASHARIKI MWADRC KUZITAZAMIA HALI HALISI YA KIUSALAMA.
SERIKALI YA CONGO IMEOMBA WAASI WA M23 KUJISALIMISHA KWA HARA KABLA HAWASHUGHULIKIWA NA JESHI LA UN MONUSCO HUKO DRC.
WAKATI HUOHUO MABALOZI 15 KUTOKA UMOJA WA AFRIKA UKIONGOZWA NA DR JORAM MUKAMA BISWARO UMETEMBELEA HUKO MASHARIKI MWADRC KUZITAZAMIA HALI HALISI YA KIUSALAMA.