GARI LA AFISA WA POLISI LAKUTWA NA MAGUNIA 18 YA BANGI MOSHI

      SIKU chache baada ya Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam kuwakamata askari 16 wakituhumiwa kujihusisha na biashara ya magendo, askari wengine wawili wa jeshi hilo wamekamatwa mkoani Kilimanjaro wakiwa na shehena kubwa ya bangi wakiisafrisha kwenda nchini Kenya.
      Askari hao walikamatwa Mei 19 mwaka huu saa nne usiku eneo la Himo, Kilemapofu, Wilaya ya Moshi Vijijini wakiwa na magunia 18 ya bangi ambayo walikuwa wameyapakia kwenye gari la Mkuu wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU) mkoani Arusha aina ya Toyota Land Cruiser lenye namba PT 2025.

No comments: