Mandhari ya Edo - Kawagoe nchini Japani.

Katika mfululizo wa makala za matembezi, leo tunatembelea nchini Japani.
Matembezi yanajikita katika mitaa ya mji wa Kawagoe inayodumisha mandhari ya Edo katika mkoa wa Saitama, ambapo unaweza kuona majengo mengi yaliyojengwa zaidi ya miaka 100 iliyopita.

Hili ni jengo la Osawa lililojengwa mwaka 1792.
Kwa miaka mingi lilitumika kama duka la viatu,
lakini siku hizi linatumika kuuza bidhaa za sanaa kwa ajili ya watalii.

Majengo mengi ya kuvutia ya mbao yenye ghorofa mbili yenye paa za vigae vyeusi, yamepangana katika mtaa ujulikanao kama Ichibangai-dori, unaoanzia kusini hadi kaskazini mwa mji.

Honmaru Goten, jengo kuu katikati mwa kasri la Kawagoe bado lipo.
Haya ni makazi ambayo mtawala wa eneo hilo alikuwa akifanya kazi na kuishi.


Mto huu ulikuwa ni njia muhimu ya usafiri wa majini kati ya Edo na Kawagoe.
Sehemu hii ilikuwa ni gati kubwa zaidi ya Kawagoe.

Viazi vitamu hulimwa Kawagoe, na kuna aina mbalimbali za viazi vitamu.
Imoyokan, au mgando wa rojo la viazi vitamu, hutengenezwa kwa kuchemsha viazi vitamu kwa mvuke, na baadaye kutengeneza mgando wa rojo hilo katika umbo la mche mstatili.

Makala yetu kwa leo inaishia hapa. Wiki ijayo tutaendelea kutembelea miji kadhaa ya Jani. Kama una maoni au lolote usisite kutuandikia. Pia unaweza kutuandikia ukiomba tutembelee wapi unapopenda wewe. Tukutane tena wiki ijayo,siku kama ya leo.

No comments: