Sheha Zanzibar, amwagiwa tindikali

Sheha wa Tumondo Mohamed Omary Said, amemwagiwa tindikali na mtu asiyejulikana na hivyo kupata maumivu makali sehemu yake ya kifua na jicho kuumia pia.
Sheha huyo alikimbizwa katika Hospitali ya Mnazi mmoja mjini Unguja ambapo alipatiwa matibabu ya dharura.
Kamanda wa polisi wa Mkoa wa Mjini Magharibi, Mukhadam Khamis, amesema chombo kilichotumika kummwagia tindikali Sheha huyo kilipatikana eneo la tukio na kwamba polisi imekichukua kwa kukichunguza kitaalam ili kugundua aliyekuwa akikitumia kwa kuangalia alama za vidole.
Sheha huyo alimwagiwa tindikali jana usiku wakati alipotoka nje ya nyumba yake kuchota maji na ndipo mhalifu huyo alipomwagia tindikali na kwamba hakuweza kumtambua.
Sheha wa Tumondo Mohamed Omary Said akiwa hospitali
 

No comments: