Jeshi la Nigeria linasema limeuwa wanamgambo 14 wa kundi la Boko Haram na kuwakamata wengine 20 Jumapili. Jumanne iliyopita rais wa Nigeria Goodluck Jonathan aliamrisha kupelekwa kwa malefu ya wanajeshi upande wa kaskazini mwa nchi kupambana na wanachama wa Boko Haram,kundi la wanamgambo ambalo linalaumiwa kwa kusababisha vifo vya maelfu ya watu katika muda wa miaka minne iliyopita.
Lakini kufikia Jumapili Jeshi lilisema wanamgambo hao 24 wa Boko Haram walikuwa wameuawa na wengine 85 kukamatwa. Baadhi ya wachambuzi wanahofu kuwa jeshi, ambalo makundi ya kimataifa ya kutetea haki za binadamu yameshtumu kwa mauaji ya kiholela na ukiukwaji mwingine, huenda likatenga watu kwa kuuwa raia pale linapowasaka wanachama wa Boko Haram.
No comments:
Post a Comment