Taarifa zilizozagaa hivi sasa katika mitandao zinadai kuwa 
aliyekuwa kamanda wa Jeshi la Polisi mkoa wa Mwanza ameuawa na genge 
ndani ya Polisi akiwemo Kamanda Polisi anayejulikana kwa jina la Muna.
       Katika tovuti ya gazeti la Jamhuri, Deo Balile anaonekana kulalamikia gazeti hilo kununuliwa kwa jumla na watu wasiojulikana.
          Kuvuja kwa siri hiyo kumetokana na mmoja wa jambazi sugu ajulikanaye kwa
 jina la Edward Malele kujisalimisha ktk vyombo vya ulinzi na kutoa siri
 zote. 
Jambazi huyu aliombwa wa genge ndani ya polisi kushiriki katika mpango 
wa kumwua kamanda Barlow. Akakataa kwa kuwa aliwahi kumfahamu kwa karibu
 kamanda Barlow. 
          Baada ya kukataa kutekeleza agizo hilo baada ya siku chache alishtakiwa 
kwa kosa la ujambazi na kuswekwa Rumande. 
Akiwa huko ndani ya wiki moja alisikia habari za kifo cha kamanda 
Barlow. Akajua akina na Muna aliowakatalia wamefanya kazi aliyoikataa 
yeye. Na alijua yuko mahabusu kwa sababu ya kukataa mradi huo.
Baada ya kukaa huko muda mrefu bila shitaka kueleweka wala mshataki wake
 huko Lupango walimua kumwaichia. Akagoma kutoka kwa sababu anajua kuwa,
 kwa kuwa amepelekwa huko ili kuficha siri hivyo, akitoka lazima 
atauawa. Baada ya muda akaamua kukubali kutoka lupango na kukimbilia 
kituo cha JWTZ huko Mwanza. 
         Huko JWTZ Alijieleza vya kutosha na wanajeshi walimwonea huruma wakampa 
Tsh 10,000/= ilie aende Bungeni huku wakiwa wamemkabidhi namba za simu 
za wabunge 2 wa upinzani ili wamsaidie. 
Kutokana na kutokuelewa kwake alipokuwa anashangaa shangaa katika eneo 
la Bunge, alikamatwa na polisi wanalinda eneo hilo. Polisi hao wakapiga 
simu Dodoma central na Mwanza. Haraka haraka mwanza wakataka arudishwe 
mwanza kwa kuwa ni jambazi sugu. 
          Hata hivyo, kwa katika kurupushani hiyo taarifa zimeshameshamfikia Pinda
 na Nchimbi ambapo gazeti linaripoti kuwa Pinda ameagiza kijana huyo 
apewe ulinzi na asirudishwe mwanza. 
Tarifa zaidi zinaema kuwa mpaka sasa amepelekwa kusiko julikana. 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
2 comments:
hv kweli unaweza kutoka mwanza hadi dodoma kwa nauli ya shs 10,000
ha haaaa! nauli ya elfu kumi kwa kuunga unga hiyo!
Post a Comment