
Rwanda imekuwa ikikana mara kwa mara tuhuma
 kuwa inahusika na 
vita DRC
Rais wa Rwanda Paul Kagame alitoa mtazamo mkali wa ujumbe wa 
kulinda amani wa Umoja wa mataifa ulioko katika Jamhuri ya Kidemokrasi ya 
Congo.
Kagame ameiambia BBC kwamba kikosi cha Umoja wa Mataifa cha askari elfu 20 
kilichopelekwa miaka 14 iliyopita, hakijafanya lolote kutatua chanzo cha 
matatizo ya Congo na wakati mwingine kimeufanya mzozo huo kuwa mmbaya zaidi.Amesema visa vya mapigano , ghasia, na watu kupoteza makaazi yao kulitishia usalama wa eneo zima.
Serikali ya rais Kagame imekana mara kwa mara tuhuma za Umoja wa mataifa na makundi ya kutetea haki za binadamu kwamba Rwanda inawasaidia wanamgambo mashariki mwa Congo.
Rais Kagame amesema kuwa kutumia nguvu kungesaidia ikiwa tu inekuwa inalenga kusaidia msimamo fulani wa kisiasa
 
 
 
 
 
 
 
 
 
No comments:
Post a Comment