USHAURI WA BURE KWA RAISI KIKWETE JUU YA BARAZA LA MAWAZIRI!

Leo asubuhi.Niko Habari Maelezo maeneo ya Posta Mpya.Nasalimiana na baadhi ya wanahabari tunaofahmiana na tusiofamahiana kwa kuwa salamu ni kitu cha bure."Nakwambia Kasyome kama ningepewa nafasi ya kumpa ushauri raisi wetu basi mimi ningemueleza kwa kipindi hiki cha mabadiliko ya baraza la mawaziri amteue waziri ambaye atawasaidia wasanii kulinda haki zao!"amemaliza ndugu yangu huyo ambaye nilikuwa nimekwenda kumwona ofisini kwake kwa mwaliko binafsi.
Hata kama ingekuwa mimi,ni lazima nishawishike kumpa ushauri rais na kumwomba juu ya yale yanayoonekana kusahaulika n akutupwa mkono.
Mfano,Maendeleo ya mkoa wa Kigoma ambao ni kama uko Burundi na sio Tanzania ukilinganisha na mikoa mingine kuthaminiwa na sera za serikali ya Tanzania na Burundi!
Sanaa na wasanii ni kama sio watanzania!
Chonde baraza hili liwe la mafanikio!!!

No comments: