NDIPO TULIPO??

Nakataa!Nasema tena nakataa!!Wala sitaki kuamini.Sio kwamba nna'chalenji'.Hapana.Niko 'siriasi'!
Haiwezekani vijana wa kitanzania (hasa wasanii) wadidimizwe kwa maslahi ya wachache.Nasema wadidimizwe nikiwa na maana kwamba,wapo watu wenye pesa zao ambao hutumia pesa hizo kuwafanya wasanii kama mitaji yao.Yaani wakishagundua kijana ana kipaji tu,kosa!Watajigamba kumsaidia kwa lugha ya 'kumtoa'.Baada ya hapo kinachofuata ni aibu!Nasema haya kwa sababu yupo jamaa yangu ambaye anatamba na vibao vikali vya musiki wa bongo.Yule aliyeimba wimbo wa-------!Jina lake linaanzia na------------.Anaishi wilaya ya Ilala.Hana kitu.Lakini waliojigamba kumtoa wana maprado na wameinua maisha yao kupitia mikataba ya msanii huyu.Inauma,hasa pale wasanii tusipoelewa haki zetu na sheria ziko vipi!
Ninachowaomba wanii ni kuungana ili kupanuana mawazo na kupigania haki na sio kuendeleza majungu.Kumbuka majungu hayajengi zaidi ya kuimarisha uadui.
Asante kwa kunisoma.Siwezi kuwa audui kwa kusema ukweli!

No comments: