HARAKATI ZA KASI YA ARI MPYA,NGUVU MPYA NA KASI MPYA NA HAKI ZA WASANII

Hali hii ya sanaa ya Tanzania inavyoendeshwa hadi sasa na vilio vilivyopo kutoka kwa wasanii juu ya baadhi ya wadau ni muhimu kuchunguzwa na kufanyiwa kazi!
Siamini kama huko serikalni hakuna mdau wa kweli anayeweza kuleta mabadaliko ya kweli katika sanaa.
Sanaa yetu hasa muziki na filamu ni ajira ambayo ni rahisi kuliko yoyote katika soko gumu la ajira duniani.
Upande wa wasambazaji wa kazi na wasanii huko ndiko vilio vilipo zaidi!
Utakuta,mfano,tepu ya filamu inauzwa sokoni shilingi 500 za kibongo,lakini msanii pale anapata shilingi 300 hadi 500 tu!Nyingine eti gharama za usafiri wakati wa usamabazaji,sijui kudabliketi na mambo mengine mengi hovyovyo lukuki!
Nchi nyingine kama Marekani wasanii ni watu ambao haki zao zinalindwa na sheria za nchi na wanaendesha maisha yao vizuri.
Sitaki kuongea mengi ambayo nadhani wadau wenzangu wemeshayazungumza kabla yangu ila ninaomba kuikumbusha serikali chini ya uongozi moto wa mheshimiwa Raisi Jakaya Mrisho Kikwete kwamba sasa wakati umefika aelekeze moto wake kunako sanaa.
Ni mengi mazuri aliyofanya na anayoyafanya raisi kwa maendeleo ya walio wengi.Binafsi nasifu na kupata imani kwamba iko siku usawa utapatikana kwenye sanaa na maisha ya wasanii wa Tanzania kuwa mazuri na kusukuma mbele maendeleo ya Tanzania.
Sina shaka kwamba siku yoyote ninaweza kutoa filamu yangu ya kwanza na ikanitoa chini ya 'umoto' wa raisi Kikwete!
Naamnini akiipatia angle hailazii damu!
Kazi nzuri,tuko pamoja.
Tanzania yenye neema,yote yanawezekana!!

No comments: