
Kuna msemo wa Kiswahili usemao; Kimya Kingi Kina Mshindo Mkuu..Sina uhakika kwamba msemo huu una maana moja au la ila naamini kwamba unafanana na ule wa Ukiona Kobe Kainama,jua anatunga sheria! Leo napenda kuihusisha misemo hiyo na kitu ninachotaka kukuletea.
Baada ya kimya cha miaka takribani mitatu,Prof.Jay anarejea tena.
Wimbo unaitwa Kama Ipo(Kupanda na Kushuka). Tofauti na nyimbo nyingi za siku hizi ambazo hugusia sehemu moja tu ya maisha yetu binadamu,Prof.Jay katika wimbo huu anakumbusha,,kuburudisha na kuweka mambo mengi sawa katika suala zima la maisha ambayo kama ujuavyo,yana kupanda na kushuka.
No comments:
Post a Comment