Chakula kupanda bei.
Niko hapa Gongo la Mboto mwisho wa lami.Kituo cha dala dala.Kwenye Cafe mpya ya MWAKIBASA CAFE(hili jina sio rasmi mwenyewe anasema ataibatiza jingine).Hapa kuna baadhi ya watu muda mfupi uliopita walikua wan lia lia juu ya kupanda kwa bei za vyakula hasa mihogo,ndizi,viazi na matunda.Hapa ni karibu na maeneo ya mashambani(Kisarawe) alkini gharama za vyakula ziko juu.Wengi wanasema tatizo ni pesa.Wafanya biashara wanajali sana pesa kuliko walaji!'Aisee yaani kila inapofika miezi kama hii hali inabadilika inakuwa ni muda mzuri wa wafanya biashara kutengeneza pesa"alisma mama mmoja niliyeongea naye juu ya kupanda kwa bei za baadhi ya mahitaji ya nyumbani.
 
 
 
 
 
 
 
 
 
No comments:
Post a Comment