Hapo zamani palitokea taifa. Taifa hilo liliitwa TAIFA LA KASYOME kwa kimombo KASYOME NATION.Raia wa taifa hili walisifika duniani kote kwa moyo wa kupenda amani na ukarimu kwa wageni.
Kijiografia Taifa la Kasyome lilipakana na mataifa ya Kenya na Uganda kwa upande wa kaskazini.Kusini lilipakana na Zambia,Malawi na Msumbiji.Burundi,Rwanda na DRC yalikuwa upande wa magharibi.
Na kwa upande wa mashariki lilikuwepo bahari ya hindi.Serikali,wafanyabiashara wakubwa,watu maarufu,viongozi wa ngazi za juu serikalini pamoja na watu wenye hadhi kama yao waliishi jijini Mzizima.Mikoani walikuwa na wawakilishi wa kukusnya kodi tu.Mzizima ulikua ni mji uliopatikana pwani ya taifa hilo.
Baadhi ya viongozi wa taifa hili walipatikana kwa kuchaguliwa na wananchi ili wawatumikie.Badala yake kazi yao ilikuwa ni kukusanya kodi tu bila kuwatumikia.
Wananchi waliambiwa makao makuu ya taifa yalikuwa Idodomya,mji uliokuwa mbali na pwani.Bila shaka viongozi baadhi wa serikali walifanya hivi ili kuwapumbaza kabisa wapiga kura walihooji iweje kila kitu kipatikane mzizima badala ya taifa zima.
Wao (viongozi) walijisikia fahari sana kutumia mfumo wa uongozi wa maneno badala ya matendo kama yalivyo mataifa mengine duniani.
Kwa mfano, mkoani KILAGOMA,mkoa uliodharaulika na sera za serikali uliokuwa magharibi mwa taifa na karibu na ziwa TANZANIA,kulikuwa na wilaya iliyoitwa KAULISULUHU.
Mkoa wa Kilagoma ulikuwa na hadhi ya wilaya ambapo wilaya ya Kaulisuluhu ilikuwa na hadhi ya kijiji.Lakini viongozi waliona wapandikize majina makubwa ili kuwafumba macho na midomo wapiga kura walioonekana kuhoji hoji masuala ya maendeleo.Wanasiasa waligundua mapungufu ya wananchi wa Kaulisuluhu.Umeme na barabara.
Walichokifanya ni kutumia kauli mbiu za uongo zilizotia moyo za awaumini suburini Yesu atarudi ili wachaguliwe wapate kula.
Na baada ya kupatiwa kula waliondoka kwenda kuishi mzizima,mji uliokuwa na miundombinu yote kama umeme,barabara za uhakika n.k.
Na hawakuwakumbuka tena waliwapa hiyo kula.Walisubiri hadi muda mwingine ulipofika wa kuomba kula.Wakawa wanajiandaa kwa kauli-mbiu mpya nzuri nzuri zaidi kwa kuzisiliza.
"Mwaka huu tutawaletea barabara ya lami na umeme!"ndivyo walivyosema kila bada ya muda kadhaa wa kuomba kula ulipofika.
Kumbuka mwaka jana walisema hivyo,mwaka juzi,mwaka juzi yake na ........!Lakini hakikufanyiki kitu.
Hadithi yangu imeisha!
Fundisho.Hadithi hii inatufundisha tutimize ahadi kwani ahadi ni deni!
No comments:
Post a Comment