Unaniambia hamlipwi mkiblogu?Siamini!

"Hivi kweli Kasyome unasema hamlipwi mkiblogu?""Aah wapi kama hamlipwi basi mimi naamini tu umekataa kuniambia ukweli!"
Hayo yalikuwa ni baadhi ya maneno ya jamaa yangu mmoja juzi.Tulikuwa tumekaa sehemu flani flani kule "ushuani"tukipunga upepo.Ilikuwa wiendi.Nikamjibu kwa kifupi sana."Tumeamua kujitolea kusaidia kujenga ulimwengu bila malipo ya kiamwonekano(non profit)!"akaendelea kukataa kata kata.
Nakwambia siku hiyo nikuwa na kazi ya ziada.Nilichokifanya baada ya hapo.Nilimwomba tusogee palipokuwa na Internate Cafe ili niongee kwa vitendo maana alinizidi kuongea.Si unajua mimi sio mtu wa kuongea sana kwa maneno tu?.Nikamsogeza kwenye mtandao.Nikaanza kazi.Kwanza nilimfungulia mtandao wa http//:www.jikomboe.com.Pili nikampeleka sehemu ya kuanza kublogu iliyokuwa kwenye mtandao huo.Tatu nikamfungulia matandao wangu.wakati huo alikuwa kimya!Baadae aliendelea mwenyewe akapekua blogu nyingi sana kiasi kwamba akasahau hadi kilichotufanya tuingie pale kefu!.Naye akavutiwa kuanza kublogu.Amependezwa zaidi na zana mpya ya kuwasilisha mawazo huru.Na sasa anasema iko siku atafungua blogu!Hongera sana ndugu yangu kwa kunielewa!

No comments: