Azania Front
Leo bwana.Nimeona niliyokuwa sijayaona!Eeh.Nikuwepo wakati mahafali ya kuwaaga wanafunzi wa Kisutu Girls Secondary School yanafanyika.Nilialikwa kama mgipa picha.Nasikitika sitaweza kuwapandishia picha yoyote.Hii ni kwa sababu amabazo ziko nje ya uwezo nilionao.Lakini naamini mtanisamehe!Tuendelee.Ikatokea baada ya mambo yote ya kwanza kwanza kumalizika ikiwa ni pamoja na kugawa vyeti,msosi ukaleta taflani!Wahusika waliotakiwa kuleta kitu hicho muhimu wakachelewa kukifikisha Azania Front.Wageni waalikwa tulifika saa mbili asubuhi.Sherehe za mahafali zikaanza saa saba mchana.Chakula kikafika amabapo saa zetu zilisomeka mishale ya saa kumi na mbili jioni!Hicho ni chakula cha mchana!Asubushi kabisa tulipewa soda moja moja.Ona kisa kilichonisukuma kuandika mada hii.Ni hivi.Baada ya chakula kufika tu.Wageni wote walicheka.Cheko la pamoja.Kumbuka mwanzo walinuna hasa baada ya kufika saa tisa mchana.Walichokifanya baada ya hapo waliingi nadani na kuanza kukimbilia sehemu kilipowekwa chakula kabla ya kuitwa.(hii ilitokea hasa kwa wanafunzi wale wanobaki-waagwa).Hadi tunaondoka eneo hilo mimi nilikuwa hoi kwa cheko.Ukitaka kupata habari zaidi kwa wale walioko bongo unaweza kufungua redio Upendo leo saa tatu usiku.
No comments:
Post a Comment