Leo nimesikia sikia!

Kutokana na tatazo la umeme na barabara linaloukabili mkoa wa Kigoma hasa wilaya ya Kasulu ambayo haina umeme kwa miaka mingi.Leo nimesikia sikia tetesi za juu juu kwamba mheshimiwa Raisi amelizungumzia hilo huko majuu wakati akiongea na wafadhili(sina hakika kwani nimesikia kupitia redio mitete!) Sisi wana-Kasulu hatujali isipokuwa kwetu umeme na barabara vimekuwa ni kama njozi tu.Hatuna mpiganiaji wala aliyetutangulia.Ni kama kifaranga wa kuku!Haya tuliyoyasikia naomba kwa Mungu yawe ya kweli!Ili tusiwe tunashangaa kuna Kasulu ikiwa kama miji mingine hapa Tanzania.

No comments: