JK AKUBALI USHAURI KUHUSU WAALIMU
Rais Jakaya Kikwete amesema kuwa kuna haja ya kuruhusu ajira za walimu kutoka katika nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki ili kuweza kupunguza tatizo la upungufu wa walimu wa sayansi na kuboresha kiwango cha Elimu ya Tanzania.
Kauli hiyo ya Rais imekuja baada ya Shirikisho la Wamiliki, Mameneja wa shule na Wakuu wa vyuo Binafsi Tanzania (Tamongsco) kumweleza kuwa walimu kutoka nchi za Afrika Mashariki wamekuwa wakilazimika kulipia dola 1,500 kwa ajili ya kibali cha kuja kufanya kazi hapa nchini.
Kikwete alisema kuwa katika mambo ambayo nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki wamekubalina katika suala la ajira ni pamoja na kila nchi kueleza ajira ambazo inazifungua na ambazo itazifunga nchini kwake.
No comments:
Post a Comment