Serikali imesema mpango wa kufanya doria za anga katika Mlima Kilimanjaro kwa kutumia helkopta, haujapata mafanikio kutokana na hali ya hewa pamoja na mazingira ya mlima huo.
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu, alisema hayo jana alipokuwa akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalumu, Betty Machangu, aliyeuliza kwa nini Serikali isitumie helkopta katika doria zake kwenye mlima huo lengo likiwa ni kuwadhibiti wahalifu.
Katika majibu yake, Nyalandu alisema kutokana na mlima huo kuwa na msitu mnene uliofunga na kuuzunguka mlima huo, miteremko, makorongo na mito iliyopo inakuwa vigumu kuona wahalifu walio chini kama doria za helkopta zikitumika.
No comments:
Post a Comment