MRISHO MPOTO


Mrisho Mpoto ni mmoja kati ya wasanii ambao Afrika nadhani inajivunia kuwa nao.Sitaki kuzungumza mengi juu yake,kwani najua wajua kama unajua unataka kumjua zaidi!Huenda ninayoyajua kwake ni machache kuliko unayoyajua wewe!Sikiliza tangazo maarufu alilocheza la FATAKI!Kisha njoo kwenye mzigo wake anaotarajia kuuingiza mwenyewe sokoni,akimlilia kaka wa mama yake(mjomba wake!)huku akisaka nauli kwa udi na uvumba ili amfuate mjomba wake huko mjini,akamweleze anachotaka kumweleza!Habari zake ntaendelea kukuletea kadri ntakavyokuwa nikizipata.

1 comment:

Anonymous said...

Mrisho Mpoto njoo Kigoma!Tunakuzimia sana huku!