Kinondoni Morocco!

Ni jumamosi."Mitaa" ya saa saba mchana.Niko kituo cha 'dola dola'sory daladala cha Kinondoni Morocco.Nakumbuka hadithi niliyoiandika ya Kinondoni Morocco ambayo hadi sasa ninandoto za kuichapisha kama kitabu.Ukweli ni kwamba kila ninapofika hapa ninaikumbuka hadithi hii.Nikupe kiduchu?Utaisoma baadae ikichapishwa!
Basi kisa hapa sio kitabu ila nataka kuelezea kimechotokea leo.
Nimekutana na mmoja kati ya waalimu wangu enzi hizo wa Bogwe sekondari.Yeye ni alikuwa pale bogwe kwa muda kabla ya kutimkia hapa dar kusaka Nondo yake ya kwanza ya education pale Mlimani.
Basi tuko hapa tuna kumbushana na kupashana zilezile za Bogwe.Baada ya kumbushana hadi stori za viboko tunaagana.Nasepa kuingia Studio za Praise kuwajibika.