Wazungu wanatuzidi akili.Wala!

Hapana.Nakataa.Tena sitaki wala nisisiki.Eti wanatuzidi akili?Ulisikia wapi?We haujui kwamba binadamu wote ni sawa.Tatizo ambalo linatufanya sisi weusi tujidharau na kuwatukuza watu wupe siujui nini hadi sasa.Lakini nahisi ni kujiona hatufai.Kwa lipi?Kwa yote.na sio wote ni wachache ambao bado wako nyuma kifikra.Kama wanatuzidi akili,wanatulisha?Au kwa kuwa watu flani wamejenga kasumba ya kuwaomba misaada yaaina flani kwa kisingizio cha kuwasaidia watu flani ahalfu misaada hiyo inaishia kuvimbisha matumbo yao na kujaa kama ball ya Chelsea,Simba au yanga?Aah inachefua pal unaposikia mtu anakwambia eti ni bora angezaliwa Ulaya mbwa kuliko binadamu bongo!Inashangaza Eeh.Haya nimeyaandika kutokana na kisa ambacho nimekiona pale Airport nilipokuwa nimekwenda kumpokea rafiki yangu ambaye ni mzungu.Huyu jamaa baada ya kufika hatukuonana mara moja.Mimi nilikua juu hotelini wakati ngege yake ikiingia uwanajani.Nilipoteremaka nikamkuta akiwa kaikati ya jamaa flani wa miraba minne wawili.Hawa jamaa walikua wanamwomba pesa!Eti kwa kuwa yeye ni mzungu na ametoka majuu basi ana mavumba ya kugawa hovyo.Mwanzo nilifikiri wale jamaa ni vibaka(hadi sasa nashawishika kuamini hivyo.Kama sio kweli Mungu anisamehe.)Baadae tuliondoka kuelekea hoteli aliyofikia na kuwaacha jamaa wale wakituangalia kwa chati!

No comments: