Bongowood.

Leo nimeamka asubuhi na mapema tofauti na siku zingine.Kila ninalofanya linaonekana kufana tu!Mbali na yote nimekutana na msanii wa siku nyingi sana wa sanaa ya maigizo hapa Bongo.Kama unakumbuka vizuri filamu ya Hujafa Hujaumbika,bila shaka utakubaliana nami kwamba kulikuwa na wasanii wawili machachari sana enzi zile akina Pwagu na Pwaguzi.Pwaguzi yeye nimeelezwa kuwa ni marehamu kwa sasa.Mungu ailaze roho yake mahali pema peponi.Amin.Yupo mzee Pwagu.Ndie niliyeonana naye.Kumbe bdo yupo kwenye sanaa.Ni mzee kiumri.Ki-muonekano,ni mcheshi,muongeaji na mpenda mizaha sana.Yaani nimetaniana naye hadi basi!Nimepiga naye picha lakini kamera yangu imeleta mushkeri kidogo ambapo siwezi kukuletea picha hiyo kwa sasa.Ila usikonde baadae ntaileta na pamoja na mazungumzo nilyofanya naye.

No comments: