Huyu Stela wa Ndesanjo vipi?

Ni siku ya jumapili saa saba mchana.Niko nyumbani,Kasulu,Kigoma,baada ya safari ndefu ya kutumia usafiri wa njia ya reli,kutoka Dar es Salaam.Usafiri ambao ukiwa ndani ya treni ya sasa(reli ya kati) unaweza kushawishika kujiuliza "uhakika wa kufika salama?" Unakuwa na mashaka mashaka kama kweli kwenda au kutoka stesheni ya 'bungeni'Dodoma (ambako kwa sasa ndiko safari za treni huanzia na kuashia,badaya ya kuanzia Kigoma au Dar es Salaam),unaweza kufika bila 'kichwa cha treni' kuzima ghafla au kuharibika kwa reli na wakati mwingine kukaa porini kwa zaidi ya siku tatu.Huwa ni usafiri wa roho mkononi style.Aah hiki sio kisa kilichonifanya niandike makala hii.Nilikuwa tu nakumbushia tatizo letu la usafiri ambalo limenitokea mimi mwenyewe.Tuendelee na kisa chenyewe. Nimetoka kanisani.Kama kawaida na ilivyo ada,kila ninapotoka kumwabudu Mungu wangu,kwenye nyumba hiho ya ibada,huwa ninapita kwa muda Chuo Cha Ualimu Kasulu(KACCU) kabla ya kurudi nyumbani na kwenda kwenye 'mitoko' ya wikendi. Hapa chuoni kuna CAFE.Napita kwa lengo la kukamilisha sehemu ya interest zangu.Kuangalia angalia mambo kwa kutumia na kwenye mtandao wa internate.Naburudika na kuingiza mpya mpya za ulimwengu mzima kwenye ubongo wangu.Ndio.Ndivyo ninavyofanya kila ninapopata muda wa ku-click. Swali:Kwa nini nipite KACCU CAFE kuchati na sio kwingine?Jibu:Kasulu nzima ambayo inaunda wilaya tatu za mkoa wa Kigoma (Kasulu,Kibondo na Kigoma) ,ina mikahawa ya kutoa huduma za mtandao (Internate Cafes) miwili tu, achilia mbali mitandao mingine lukuki inayotumiwa na ofisi na maofisa wao. Ni huu ninaoupendelea zaidi (KACCU CAFE) na ule wa Chuo cha Biblia uliko kanisa la Anglican ambalo ninaabudia.Eeh kwa nini nisitumie kefu ya kanisani kwangu?Nitakujibu siku nyingine,kwa leo tuongelee hii KACCU CAFE. Tayari ni saa saba na dakika ishirini na mbili,inakimbilia ya ishirini na tatu.Hii ni kwa mujibu wa saa iliyorekebishwa na hawa wenyeji wa hapa (wahudumu) muda mfupi uliopita,kwenye kompyuta (tutumie jina la ngamizi) kubwa nyeusi na isiyokuwa na vifaa vyote,iliyo mbele yangu.Ninayoitumia kwa sasa. Cafe hii ina vyumba viwili vya kutolea huduma.Ni kama vilitumiwa as madarasa mwanzoni kabla ya mradi kuanza.Viko katika jengo moja lenye vyumba vitatu vya madarasa,nyuma ya jengo kuu la utawala. Madirisha makubwa ya mbao yenye vioo na pazia zilizofungwa kiustadi ndio yanayoingiza na kutoa hewa ndani.Kwa kesi ya mwanga,umeme unafanya kazi yake sawasawa.Hata kama usingekuwepo,hamna giza.Ndani haman feni wala air-condition.Hamna joto kama lile la Dar es Salam (Tanzania-kama wakazi wengi wa mikoa ya magharibi wanavyoita.Sielewi kwa nini.) Ndani ya chumba nilicho mimi kuna ngamizi (napenda kutumia neno hili badala ya kutohoa lugha ya kigeni-kompyuta) zaidi ya saba.Network inatia moyo.Wateja wanafanya mambo pamoja na kwamba kuna wakati jenereta inayotumika kuzalisha ememe,huzimika.Si unaelewa mambo ya mikoani?Haujafika!Basi hali hii na nyingine za kukela, ya kawaida tu!Lakini kastamazi sio wengi humu ndani.Naona gamizi nyingine ziko wazi. Ngamizi jirani na hii ninayoitumia,inapata mtumiaji.Amekuja mteja wa kike.Wahudumu wanamkaribisha vizuri.Na wanamwelekeza kuja kutumia ngamizi ambayo iko upande wa wangu wa kushoto.(hapa ngamizi zimepangwa katika safu mbili.Ya kulia na kushoto.Katika kila safu kuna ngamizi mbili mbili).Ni demu mdogo mdogo hivi.Kiumri kwa kumkadiria,hazidi 18 years.Anaonekana kama mwanaskonga (mwanafunzi),tena wa sekondari.Ndio.Pamoja na kwamba leo ni jumapili siku ya mapumziko (ninavyoelewa mimi),amevaa sketi ya rangi ya njano yenye malinda makubwa makubwa na amechomekea tisheti yake nyekundu.Kifuani upande wake wa kushoto kuna maandishi makubwa yaliyokorezwa kwa wino mwekundu"EDUCATION FOR EXCELLENCE".Lakini jina la shule kwenye ile t-shirt sikuipimia fasta.Sikuliona kwa sababu maandishi mengine yalikuwa magodo madogo sana na sikuwa na taim naye.Nilibahatika kuyaona hayo mengine sababu yalikuwa makubwa na yalilandana na mavazi yake. Wakati huo mimi nilikuwa nasoma kisa cha STELLA kwenye mtandao wa http://www.jikomboe.com/. "Mambo vipi brother!"alinisabahi. "Poa"nilimjibu kwa makato bila hata kumwangalia, nikiwa nimekazia macho kwenye ngamizi yangu.Sijumbuki ilitokea nini?Akaangalia kwenye kioo cha ngamizi niliyokuwa naitumia.Nikageuka kumwangalia usoni.Naye akaniangalia.Tukakutanisha macho.Wote kwa pamoja tukatabasamu.Baadaye yeye alicheka kabisa!Akinamisha kichwa chini.Ni aibu ya kike? "Unajua kitu kaka?"aliuliza,baada ya kucheka sana. "Siju!"nikamjibu. Alicheka sana hadi machozi yakawa yanamtoka!Nikamwangalia kwa chati,bila kuelewa anamaanisha nini.Nikiwa bado namsoma.Akaanzisha tena. "Mimi pia naitwa STELLA!"alisema kwa pozi. "Kwani wewe hauna Stella?"aliniuliza haraka haraka nikiwa bado sijaongela lolote,tangi alipoanza kucheka! Unafikiri nilimjibu?Sikumjibu.Nikajifanya niko bize sana.Najua alikuwa na uhakika wa kwamba swali lake nililisikia na kulielewa.Unajua nini kilifuatia?Hakutaka kufuatilia zaidi.Kwa upole na taratibu akahamia kwenye ngamizi yake.Akafanya kile kilichomleta.Yakawa yameisha. Sio kwamba sikufurahia mazungumzo yake.Hapana. Niliyafurahia.Tena kwa sana tu.Tatizo muda ulikuwa hauniruhusu na mahala pale hapakuwa mahala pake! Baadaye nitakuletea sehemu ya pili ya kisa hiki. Kama haukifahamu kisa cha Stela nilichokuwa nasoma,fungua www.jikomoe.com/?p= Hii hapa ni picha ya KACCU CAFE

No comments: