
Je,ni zipi hizo?...Ni zile alizozinena Tanzania katika sura ya ishirini ya kitabu cha Blogu,akisema;
1.Usiwe mbishi kama Zitto Kabwe,kwani kopi mpya ya CD,ya tamthilia ya kuvutia,isiyo na mwisho,ya kundi la sanaa la CCM (yaani Chukua Chako Mapema),hautapewa kama zawadi.
2.Usiwe muuaji kama Ditopile,kwani nawe hautauawa.
3.Usiwe na tamaa kama Lowassa,kwa kutamani kupokewa kama shujaa jimboni.
4.Usiwe mwongo kama Karamagi,kwani Richmond na EPA hawatatokea.
5.Usiwe mwizi kama Balali,ili baadae usijifiche.
6.Usiwe mziba masikio sana kama kaka wa mama wa Mrisho Mpoto.
7.Usilie bungeni kama Pinda,ukapindia machozi.
8.Usihukumu kama Kisutu,kwani nawe hautahukumiwa.
9.Usiwe mmiliki wa fujo zenye makelele kama Makamba.
10.Ona huruma kama Dr.Slaa ili siku zako za kuishi zipate kuwa nyingi katika nchi uliyopewa.
No comments:
Post a Comment