Ni maendeleo au wizi wa kiteknolojia?

Jana jioni shemeji yangu kapata sms kwenye simu yake ya mkononi.Sms hiyo ilimtaarifu kuwa ameshinda bahati nasibu ya kimataifa.Mamilioni ya pesa!Ikaendelea kusema kuwa anatakiwa kutuma shilingi elfu 5000(elfu tano)za kibongo ili iwe processing ya kutumiwa mamilioni hayo.Sms hiyo ilionesha kutoka kwa wenzetu wa nchi jirani.Ambapo ukiwatumia hiyo elfu tano kwao ni pesa nzuri.Cha ajabu akaja jirani yetu naye akiwa ametumiwa sms ya namna hiyo siku mbili zilizopita.Akatuma kiasi alichoambiwa kupitia namba ya akaunti ya benki iliyoamabatana na sms aliyotumiwa.Lakini hadi sasa hajatumiwa pesa zake!Bila shaka huo ni wizi!Sina hakika.Lakini kuwa makini.

No comments: