Mishemishe za Dar

Niko maeneo ya Kariakoo.Wakakti nakuja hapa nilipita Mnazi mmoja.Kuna vijisemu wanuza uza chakula(mama lishe).Walivyojipanga unaweza kufikiri labda ni zile squire za majuu!Tatizo lao moja tu.Hawa wanakuwa na wakakti ambo wanawachangamkia wateja na wakati ambao wanawanunia!Eeh.Nilipita pale nikasikia sauti ikinikaribisha kabla sijafika."karibu kaka..."Wanakua shap kweli kiasi kwamba wanauhakika unakwenda kuapata huduma.Wakati naendelea mbele bila kuwajibu kwa kuwa lengo langu lilkuwa sio huduma yao.Nikasikia wakimfokea mmoja wa wateja wao."kama hauwezi utoke hapa ohoo!"Sikuelewa walimaanisha nini wala hakuweza nini yule mtu.Nikaendelea na hamsini zangu!

No comments: