Imenikumbusha enzi zileeee!
Hivi ni mkweli serikali imeusahau mkoa wa kigoma?Zito Kabwe aliongea kitu flani siku moja bungeni(sikumbuki ni siku gani hasa kwa kuwa sikuwa makini sana siku hiyo).Aligusia eneo la uwakilshi wake kule Kigoma kaskazini.Mimi nimekumbuka suala la maji,simu,umeme na barabara za uhakika.Hapa tuaongelea zaidi barabara na umeme ambavyo vimekuwa kero kubwa kwa wakazi wa mkoa wa Kigoma.Kwa upande wa wilaya ya Kasulu Mh.Zitto Kabwe hahusiki.Kule tunaye mwakilishi wetu akatika bunge.Nitawazungumzia wote wanaohusika na kuwawakilisha wananchi wa wilaya nzima ya Kasulu, sio mbunge wa Kasulu mashariki pekee ambaye anadhamana kubwa kwenye baraza la mawaziri la sasa.Wananchi wa wilaya ya Kasulu wanashukuru kwa kuwa huwa anakwenda kuwasalimia tu na sio kingine!Yaani baada ya vikao vya bunge kule Dodoma na kurudi Dar huwa anapata muda wa kwenda kuwaona wapiga kura wake.Akifika sasa.Anawakumbusha machungu yao ya kila siku.Umeme na barabara ya lami.Kila kukicha wanasiasa wanapofika Kasulu wanachochea maneno kama cherehani. Yanayowalainisha wapiga kura wao na kubaki mikono ikipiga makofi na midomo kushangilia kila kinachosemwa!Suala hapa ni umeme na barabara tu.Juzi juzi kwenye kampeni wananchi waliahidiwa ahadi yao ya muda mrefu kwamba kabla ya muda wa uwakilshi kuisha Kasulu itakuwa inawaka usiku badala kutumia vibatari na majenereta yanayochafua hali ya hewa na kusababisha makelele mitaani (hata hivyo ni kwa wenye nazo na watu wengine wenye hadhi kama yao!)Ukipita mitaa ya Murubona hadi Murusi kuanzia Kagunga utakuta ,ilingot ya umeme.Hii ilisimikwa enzi zile za uchaguzi wa mwaka 2000.Lengo hapa lilikuwa ni kuvuta hisia za wapiga kura ili wapate hawa wanasiasa wapate 'kula' badala ya kura!Nasema hivyo kwa sababu.Moja hatujaona lolote lililotendeka baada ya uchaguzi ule.Pili hakuna umeme ulioletwa hadi sasa pamoja na kwamba iliahidiwa kuwa baada ya uchaguzi na mhusika kushinda basi umeme ungepatikana na barabara ya uhakika ya kupitika muda wote ingewezeshwa.Kweli mhusika alishinda na akahamia huku dar.Sijui alisahau ahadi zake au la.Naandika hivi kwa sababu imenigusa baada ya kukumbuka t-shirt niliyopewa juzi juzi inayofanana na enzi zile ya kasi mpya.nguvu mpya na ari mapya!Maisha bora kwa kila mtanzania!Hivi ni kweli?Mbona hakuna ubora wowote wa maisha kwa wananchi wa Kasulu badala yako wanazidi kulia nauli za basi kupanda bei.Siku za nyuma nauli kutoka Kasulu kwenda Kigoma mjini ilikuwa ni shilingi za ki-Tanzania 300.Lakini kwa sasa ni sh.600!Mara mbili yake.Au hii ndio kauli mbiu ya maisha bora kwa kila mtanzania?.Hapa wanofaidi ni wale ndugu zao na wanaofanana na wao tu.Mwananchi wa kawaida ni shida tupu.Naomba tukumbukwe.Jana jioni nilsikia sikia tetesi kwamba wanchi wa mkoa wa Kigoma wemebaguliwa na serikali yao.Nilisikia kwa mfanya biashara mmoja wa kimataifa wa raia wa DRC.Huyu alikuwa maeneo ya Kariokoo.Nilipomsikia iliniuma sana.Ikabidi niondoke tu kimya kimya eneo lile.Sasa kama hata wageni wanfikra kama hizo.Je anayedanganywa?Afike wapi?Eeh huu ni uongo.Kwani anaye sema uongo anaitwa nani?kikisemwa kitu ambacho sio kweli nini maana yake?Au ndio kusema mkoa wa Kigoma uko kwingine na sio Tanzania?Au hatuna mwakilishi wa kweli bungeni?Cha kushangaza tunachagua wenyewe na kupigwa chenga wenyewe!Kuanzia enzi zile za kusimikwa nguzo za umeme hadi sasa mwakilishi bado ni wa CCM tu.Kitu ambacho bado hakina mabadiliko kabisa kwa wilaya ya Kasulu.Nazungumzia Kasulu sana kwa sababu ninaifahamu.Nimezaliwa pale.Nimekulia pale.Nimesoma pale.Nimekuja huku tu kwa sababu za kiutafutaji.Na hii haiwezi kuwa sababu ya mimi kuwapiga chenga ndugu zangu.Ntasema tu.Kama noma na iwe noma!Naomba wahusika wawaangalie wapiga kura wa Kasulu.Wanahitaji kusihi kama walivyo wapiga kura wengine kutoka sehemu nyingine za Tanzania.Wa-Tanzania wote ni sawa.Wana haki sawa kwa kila kitu.Iweje mahali flani kuwe tofauti na kwingine.Tunaomba tutendewe haki.Ninaimani ujumbe umefika.Asante kwa kunisoma!
No comments:
Post a Comment