Special kwa washkaji wanaotaka kwenda kukamua majuu.

Kwa wale wanaotaka kwenda kusoma majuu (Ulaya,Marekani,Australia n.k) katika vyuo.Elimu ya sekondari kwetu Bongo haitambuliki katika misingi ya shule za Ulaya! Shurti ujaribu kumaliza shahada ya mwanzo (Bachelors) au Diploma halafu ukaanza kuomba au kutafuta kusomea zaidi vyuo vya majuu. Ukiamua kujilipia unaweza kusoma popote na chochote utakacho.Kwa wastani ada ya mwaka kwa shahada ya mwanzo kama sijakosea ni shilingi za kitanzania milioni kumi.Kwa mwafrika wa kawaida ni vigumu sana kumudu gharama hizo.Wanachofanya wengi ni kwenda na pesa zao (nauli ya ndege wastani wa shilingi laki nane) wakajiandikisha katika vyuo,wakawa wanajilipia kwa kufanya kazi za usiku.Unasoma mchana huku ukichapa kibarua usiku.Wasomi wa Afrika Ulaya wanamenyeka sana kujilipia.Hakuna cha bure majuu! Kuna njia nyingine nyingi za kujiendeleza kielimu.Kama kujiandikisha katika masomo ya barua kwa njia ya posta au mtandao.Unaweza kufanya yote haya ukiwa hapo hapo ulipo.Chuo maarufu cha Cambridge International College (CIC) na International Correspondence School (ICS) ni mfano mzuri. Je,utavijuaje vyuo vya aina hii ambavyo ni vingi?Siku hizi kila kitu kiko katika mtandao.Fungua ukurasa wangu wa SCHOLARSHIPS au nenda katika web la google tafuta neno lolote utakalo.www.google.com
Nimeitoa kwa Freddy Macha.

No comments: